UTANGULIZI
Jumuiya ya taalim old students imeanzishwa rasmi mwaka
2015.Ikiwa ni jumuiya iliyowakusanya wanafunzi waliosoma madrasat taalim
Islamic foundation ambao wenye nia ya kuendeleza madrasa yao(taalim Islamic
foundation)
Taratibu za jumuiya hii ya taalim old students
zimeandikwa katika katiba hii na ndizo ambazo zitakazotumika kama mwongozo wa
jumuiya katika mambo yote yahusuyo uendeshaji wa jumuiya.
Katiba hii imepitishwa kwa kauli moja na makubaliano ya
wanajumuiya wote waanzilishi na kila mwanajumuiya atakayejiunga na jumuiya hii
atawajibika kuisoma katiba hii na kuifuata.
SEHEMU YA KWANZA
1. JINA LA JUMUIYA NA MAKAO MAKUU
a)
Jina la jumuiya ni taalimu old students amabalo
kifupi chake ni T.O.D
b)
Makao makuu ya jumuiya yapo Mwananyamala
komakoma wilaya ya kinondon mkoa wa Dar es salaam
2. MALENGO YA JUMUIYA
Lengo kuu la jumuiya ni kusimamia na
kuendeleza madrasa yetu (taalim Islamic foundation) kwakuboresha mfumo
wautolewaji waelimu na kupambana na changamoto mbalimbali zinazoikabili madrasa
yetu. Pia kukipa nguvu kituo chetu(madrasa) na kukifanya kuwa kituo endelevu
kitakachokuwa kikitoa huduma ya mafundisho ya elimu ya dini yetu ya kiislam.
3. MIKAKATI YA JUMUIYA KATIKA KUENDELEZA MADRASA
A) Kuboresha mfumo wa elimu
- Jumuiya
itahakikisha wanafunzi wanasoma kwa kufuata silabasi iliyoandaliwa na walimu.
- Pia kila mwanafunzi atapatiwa elimu bora
ambayo itamjenga kiimani na kujitambua
- Kuandaa mashindano ya kuhifadhi Qur-an na
kusoma tafsir ya Qur-an kwa wanafunzi na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya
vizuri ili kuwahamasisha vijana wetu wapende kusoma na kuilewa dini yao.
- Pia jumuiya itakuwa ikifanya mikutano ya
mara kwa mara baina ya walimu na wazazi ili kujadili maendeleo ya wanafunzi.
B) Posho za walimu
- Jumuiya imeweka mikakati maalum ambayo
itawawezesha walimu wa madrasa kupatiwa posho ili kuwafariji na kuonyesha kuwa
tunajali kwa kile wanachokitoa kwa wanafunzi wetu.
C) Usimamizi wa mazingira ya madrasa
- Jumuiya imeweka taratibu za
kujenga/kurekebisha jingo la madrasa pindi jingo litakapokuwa linahitaji
kufanyiwa marekebisho ili kuimarisha jingo hilo la madrasa lisiwe chakavu.
- Pia jumuiya itahakikisha mazingira ya
madrasa yanakuwa katika hali ya usafi na yenye kuridhisha.
SEHEMU YA PILI
1.
UANAJUMUIYA
Katika jumuiya yetu kutakuwa na wanajumuiya wa aina mbili kama ifuatavyo
A)
Wanajumuiya waanzilishi- hawa ni wanajumuiya
ambao walioshiriki kikamilifu katika hatua zote za mwanzo za uanzilishi wa
jumuiya.
B)
Wanajumuiya washiriki- hawa ni wanajumuiya ambao
watapitishwa na kuwa wanajumuiya baada ya kujaza fomu maalum ya maombi ya
kujiunga na jumuiya.
2.
SIFA ZA MWANAJUMUIYA
A)
Awe muislamu na mwenye kufuata mwenendo wa
uislamu
B)
Awe tayari kutii mwongozo (katiba)
C)
Awe mwenye akili timamu
D)
Awe baleghe
3.
HAKI NA WAJIBU WA MWANAJUMUIYA
A)
Kuhudhuria vikao vyote vya jumuiya
B)
Kulipa ada ya kila mwezi na kwa wakati
unaotakiwa
C)
Mwanajumuiya ana haki ya kutoa maoni yake katika
vikao vya jumuiya na kusikilizwa.
D)
Mwanajumuiya anawajibika kuchangia kiasi
kitakachopangwa na jumuiya kwa ajili ya kutoa pongezi au kumfariji mwanajumuiya
ambae anastahiki kupewa pongezi au faraja kwa wakati huo.
E)
Pia mwanajumuiya anatakiwa kushiriki katika
shughuli zote za jumuiya zikiwemo sherehe mbalimbali au msiba.
4.
MICHANGO KWA WANAJUMUIYA
Mwanajumuiya anatakiwa kuchangia kiasi cha fedha kitakachopangwa na
jumuiya kwa mwanajumuiya yoyote atakayefikwa na lolote kati ya haya yafuatayo-
A)
Mwnajumuiya atakayekuwa anahitaji kuoa aua
kuolewa
B)
Mwanajumuiya atakayepatwa na maradhi na kulazwa
hospitali kwa siku tatu mfululizo
C)
Mwanajumuiya pindi atakapofiwa na ndugu yake
yoyote kati ya baba,mama,mke,mme,mtoto au ndugu wa damu katik,a familia.
5.
MAMBO YANAYOPELEKEA KUPOTEZA UANAJUMUIYA
A)
Uanajumuiya utakoma pindi mwanajumuiya
atakapoamua kujitoa na kutojihusisha na jambo lolote linalohusu jumuiya
B)
Aidha uanajumuiya utakoma baada ya kamati ya
jumuiya kuamua kumvua uanajumuiya mwanajumuiya amabae anakwenda kinyume na
katiba.
C)
Pia uanajumuiya utakoma pindi mwanajumuiya
atakapofariki.
SEHEMU YA TATU
1 1. SHERIA NA TARATIBU ZA JUMUIYA
A)
Nidhamu.
-Kila mwanajumuiya anatakiwa kuwaheshimu viongozi pamoja na wanajumuiya
wenzake
-Pia kuheshimu mawazo au maoni ya kila mwanajumuiya.
-Kuzingatia utaratibu maalumu wa chumba cha kikao, mfano; hairuhusiwi
kuzungumza pasi na ruhusa ya mwenyekiti au kufanya mawasiliano ya simu ispokuwa
kwa waliopewa idhini na uongozi.
B) Kutohudhuria kikao/kuchelewa ni
kosa la jinai.
-Mwanajumuiya yoyote ambaye atohudhuria kikao pasi na kutoa taarifa kwa
uongozi atatozwa faini ya shilingi 1000/= ikiwa ni kama sehemu ya adhabu.
-Pia kwa atakayechelewa kuhudhuria kikao pasi na kutoa taarifa kwa
uongozi nae atatozwa faini ya shilingi 500/= kama sehemu ya adhabu.
C) Kuchangia fedha kwa ajili ya
maendeleo ya jumuiya.
-Kila mwanajumuiya anatakiwa
kuchangia kiasi cha shilingi 2000/= kwa kila wiki au shilingi 8000/=- kwa kila
mwisho wa mwezi
N.B
*Kiwango cha uchangiaji
kinaweza kubadilika kulingana na wakati
*Kila mwanajumuiya anatakiwa
kuwa tayari kuchangia michango ya dharura
D) Stara
-Kila mwanajumuiya anatakiwa kuvaa mawazi yanayokubaalika katika sharia
ya uislamu.(mwanamke anatakiwa kufunika mwili wake wote ispokuwa uso na viganja
vya mikono na mwanaume anatakiwa kufunuka maeneo yaliopo kati ya kitovu na
magoti).
-Mwanajumuiya atakayekiuka vazi la stara atatolewa kwenye chumba cha
kikao na kutozwa faini ya shilingi 2000/=
E) Umoja na mshikamano.
-Kila mwanajumuiya anatakiwa kujiepusha na jambo lolote litakaloashiria
kupoteza umoja na mshikamano wa jumuiya.
SEHEMU
YA NNE
1.
UONGOZI WA TAALIM OLD STUDENTS
A)
Mwenyekiti na naibu mwenyekiti
B)
Katibu na naibu katibu
C)
Mweka hazina
D)
Afisa habari
E)
Wajumbe
2.
KAZI ZA VIONGOZI WA TAALIMU OLD STUDENTS
A)
Kazi za Mwenyekiti
-Kuongoza vikao vya T.O.D na kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya jumuiya
-Kupokea taarifa mbalimbali za wanajumuiya
-Pia atakuwa msemaji wa jumuiya
B)
Kazi za katibu
-Kuandika na kutunza kumbukumbu za vikao vya jumuiya.
-Kutoa taarifa za maendeleo ya jumuiya
-Kuratibu shughuli za mapato na
matumizi ya jumuiya
-Kutunza kumbukumbu na taarifa muhimu za wanajumuiya wote.
-Kuitisha vikao vya jumuiya kwa kukubaliana na mwenyekiti.
C)
Kazi za mweka hazina
-Kutunza fedha za jumuiya
-Kuandaa taarifa za mapato na matumizi ya jumuiya kila mwisho wa mwezi.
D)
Kazi za afisa habari
-Kutoa taarifa za kuitishwa vikao kwa wanajumuiya baada ya kujadiliana na
kukubaliana na viongozi wenzake.
-Pia kutoa taarifa za yaliyojadiliwa katika kila kikao kwa wanajumuiya
wote.
E)
Kazi za wajumbe
-Kutetea na kusimamia maslahi ya jumuiya.
3.
MUDA WA UONGOZI MADARAKANI
-Viongozi wapya watateuliwa kila baada ya miaka mitatu.
-Uongozi uliopo madarakani unaweza kuendelea na madaraka ikiwa ni
waadilifu na wanakubalika na wnajumuiya wote.
-Kiongozi
huenda akavuliwa madaraka ikiwa ataonekana hafai kwasababu za msingi kwa mfano,
kuvunja katiba ya T.O.D, kutumia madaraka vibaya au kutumia jina la jumuiya kwa
manufaa yake binafsi.
SEHEMU
YA TANO
1.
VYANZO VYA MAPATO
Jumuiya ili iweze kuendesha shughuli zake mbalimbali inategemea mapato
kutoka kwenye vyanzo vifuatavyo.
A)
Ada ya kila wiki au kila mwisho wa mwezi
inayolipwa na kila mwanajumuiya
B)
Faini zinazotozwa kwa wanajumuiya ambao
wanachelewa au kutohudhuria vikao.
C)
Pia miradi mbalimbali itakayoanzishwa na
jumuiya.
2.
UDHIBITI WA FEDHA ZA JUMUIYA
A)
Fedha za jumuiya zitahifadhiwa benki katika
akaunti ya jumuiya
B)
Fedha za jumuiya hazitatolewa benki ispokuwa kwa
makubaliano ya wanajumuiya wote wakiongozwa na mwenyekiti.
Aaamin
ReplyDeleteKatka uongoz wa jumuiya tungefurah zaid endapo tungepata na liongozi wa nidhan ili kuweza kucmamia maswala yote ya nidhamu kuanzia nidhamu za kikaoni na kuendelea kupata muendelezo mzuri wa kila jambo litakalofanyika.
Inshaa allah
insha allah atapatikana tu ndg yng@ibrahim yusuph
Delete